Frontrunners ni nini? ni nini?

Frontrunners ni nini? ni nini?

"Frontrunners" ni yenye maana ya (Waongozaji, viongozi, watu walio mstali wa mbele kuongoza wenzao) ni Programu ya Kimataifa ya Mafunzo ya Viziwi juu ya Uongozi wa Vijana inayolenga Miradi ya Utawala ya Kimataifa.

Lengo ni kuwafanya viziwi walio na moyo na uwezo wapate uwezo mkubwa wa kuyageuza maisha ya viziwi kuwa mazuri.

Washiriki wa Frontrunners wanatoka duniani kote, wakiwa na umri kuanzia miaka 18 hadi 30. Wote wanaojiunga na programu hii wana malengo ya baadaye kwa faida ya viziwi. Tukiwa kama watu binafsi tuna uwezo wa kuboresha hali za maisha ya viziwi katika nchi zao na duniani kote. Lengo kuu la Frontrunners ni kuwa na dunia bora.

Frontrunners 2007 ni kozi ya tatu. Ya kwanza ilikuwa mwaka 2005 na ya pili mwaka 2006 ambazo ziliendeshwa kwa miezi minne tu.

Programu yetu ya Frontrunners kwa mwaka huu imeongezwa muda wa mafunzo kuwa miezi nane. Imegawanyika katika vipindi mihula yenye miezi mitatu.

Katika muhula wa kwanza, washiriki hujifunza dhana ya Frontrunners, ambayo ndiyo somo kuu - Uongozi na Usimamizi wa Miradi -, pamoja na topic nyingine kuhusu utambulisho, saikolojia, sosholojia, siasa, utamaduni, lugha, masuala mengine yakiwamo ukaguzi, Uchangishaji fedha, Uziwi, uwezeshaji, Nchi Zinazoendelea, etc.

Somo kuu litaendeshwa kwa vitendo wakati wa muhula wa pili. Tutaunda miradi yetu wenyewe. Inaweza kuendeshwa nasi wenyewe au katika nchi yoyote.

Katika muhula wa mwisho, tunarudi katika miradi yetu. Somo kuu ni kutambua udhaifu na uwezo juu ya uzoefu katika kazi yetu kuanzia wakati wa muhula wa pili na kutathmini kila somo tulilopitia.

Tunategemea kwamba programu hii itatuletea faida. Tufuate! Kwanini? Tutafanya mabadiliko ya ripoti katika tovuti hii kila wiki. Hivyo toa kipaumbele!

Navigation

Problems?